Confession #588

#588 76

Kuna confessions za madada fulani humu ndani zinanikera sana. Zaudhi kabisa. Dada Yangu Hatakama Mume wa Mtu Anakwambia Anakupenda Kuliko Mke Wake Hata Siku Moja Hawezi Kumwacha mke wake akuoe wewe. Yaani Ukiona Mwanaume Kamwacha Mke wake akaenda Kuuweka ndani mchepuko wake basi Jua kwamba sio Akili yake ni akili ya Kupewa. Ninacho jaribu kukwambia leo hii dada Yangu ni kwamba achana na mume wa Mwenzio Tafuta wa kwako. Yaani vijana kibao wanakutongoza Unawakatalia unasema Tayari Unamtu Mtu Mwenyewe Mume wa mwenzio hivi Unaakili kweli wewe?? Acha kuringa na mali ambayo sio yako. Kama kakwambia mke wake Anamsumbua unadhani ni ukweli anacho kisema? Kama alikuwa anajua mke wake ni msumbufu kwanini alikubali kumwoa?? Anakulalamikia kwamba mke wake hampi sex hao watoto Walionao wamewapataje? Ebu amka usingizini Dada najua ukweli uchungu…..🤣🤣

May 17, 2020 |
6
0
Your Comment has been sent
Your Comment is too short
2000 characters left